
Na Mwandishi wetu WAMACHINGA DAR ES SALAAM
Sakata la tuhuma za harufu ya ufisadi na rushwa katika vibari vya sukari lililoibuliwa na Mbunge wa kisesa Luhaga Mpina limeendelea kuzua mjadala na kuwaibua watu wa kada mbalimbali kuzungumzia sakata hilo,
Mchambuzi wa maswala ya uchumi na siasa Kassim Kibao ameibuka na kuzungumza na waandishi wa habari juni 9,2024 jijini Dar es Salaam na kusema kuwa Waziri Hussein Basheย hakutoa vibari kwa mkono wake bali vibari vya kuagiza sukari vilitolewa kupitia Wizara ya Taifa ya Chakula NFRA
Kibao ameongeza kuwa kampuni iliyotajwa na Mpina ya Mohammed Enterprisesย ni kampuni inayojihusisha na biashara zaidi ya moja na kama kampuni inavibari na imesajiliwa sio kosa kama ikiruhusiwa kuingiza sukari nchini.
“Mambo yanayo amriwa na bunge yaachwe yaamliwe na bunge yasitoke nje ya bunge,Mpina amekosea kutoka na ushahidi nje ya bunge hatujui dhamira yake ni nini,na kufanya hivyo ni kumshinikiza spika,ninaimani kamati ya maadili ya bunge itatenda haki iwapo ushahidi wa mpina utakuwa upo Sawa na iwapo anapotosha na kuzua taharuki atachukuliwa hatua”Amesema Kibao.