Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania imeandaa mfumo mpya ya Teknolojia ya kujiandikisha Katika daftari la kudumu la mpiga kura Kwa kutumia njia ya mtandao
Ameyasema hayo Leo Tarehe 13 Juni 2024 Mwenyekiti wa Tume Mhe.Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele wakati akifungua kikao kazi Cha waandishi wa habari kilichofanyika Mlimani City Jijini Dar es salaam
Amesema sambamba na mabadiliko ya Teknolojia ikiwa ni pamoja na kurahisisha Zoezi la uboreshaji wa Daftari,imeboresha mfumo wa uandikishaji ambao Kwa mara ya kwanza utamwezesha mpiga kura aliyepo kwenye Daftari kuanzisha mchakato wa kuboresha taarifa zake au kuhama kituo Kwa kutumia simu au kompyuta.na baadae kutembelea kituo anachokusudia kujiandikisha Ili apatiwe kadi yake ya mpiga kura
Aidha Amesema kifungu Cha 9(1) na (2) Cha sheria ya uchaguzi wa Rais,Wabunge na Madiwani Na 1 ya Mwaka 2024 uboreshaji wa Daftari utahusu watu wote wenye sifa za kuandikishwa kwenye Daftari la kudumu la wapiga kura
“Tume imeweka utaratibu Kwa watu wenye ulemavu,wazee,wagonjwa,wajawazito na wakina mama wenye watoto wachanga watakaokwenda nao vituoni kupewa fursa ya kuhudumiwa bila kupanga foleni”Amesema Mwambegele
Aidha amebainisha kuwa Tume Chini ya kifungu Cha 10(1)(g) Cha sheria ya tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Na.2 ya mwaka 2024,imepewa jukumu la kutoa elimu ya mpiga kura nchini
Hata hivyo Amesema Katika kutekeleza jukumu hilo,imejipanga kuhakikisha kuwa wananchi wanapata uelewa.wa kutosha Kuhusu uboreshaji huo
“Njia mbalimbali za kutoa elimu ya mpiga kura zitatumika Ili kuhakikisha kwamba wadau wote wanapata fursa ya kuelimisha na kuelewa mambo yote ya msingi Kuhusu uboreshaji huu Ili wajitokeze Kwa wingi kushiriki kwenye Zoezi hilo”. Amebainisha Mwambegele
Zoezi la uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura linatarajiwa kuzinduliwa Tarehe 01 Julai 2024 Kigoma na Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa