119 views 56 secs 0 comments

TAWA YANG’ARA MAONESHO YA UTALII NA BIASHARA TANGA

In KITAIFA
June 07, 2024

Na Beatus Maganja TANGA

Yanyakua tuzo na kujikusanyia vyeti kadhaa vya pongezi*


Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania – TAWA imepokea tuzo ya mshindi wa pili wa jumla kwenye maonesho ya  11 ya utalii na biashara almaarufu “TANGA TRADE FAIR” yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja vya shule ya sekondari usagara Mkoani Tanga  kuanzia Mei 28, 2024 mpaka Juni 06, 2024.

Sambamba na tuzo hiyo, TAWA pia imetunukiwa vyeti vitatu kwa ushindi  na  pongezi kwa kushiriki na kufanikisha maonesho hayo.

Tuzo na vyeti hivyo vilitolewa Juni 06, 2024 na  Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Dkt. Batilda Buriani ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa hafla ya kuhitimisha maonesho hayo kwa Mwaka 2024 ambapo taasisi mbalimbali za Serikali na zisizo za Serikali zilishiriki.

Licha ya kujikusanyia tuzo na vyeti mbalimbali vya pongezi, TAWA pia imepongezwa kwa kufanikisha uwepo wa wanyamapori hai ambao walikuwa   kivutio kikubwa na hamasa ya watu wengi kuhudhuria na kushiriki katika maonesho hayo.

TAWA imeshiriki kikamilifu maonesho hayo ya biashara na utalii yaliyokuwa na  kauli mbiu *”Kufungua fursa za kiuchumi kupitia ushirikiano wa Sekta za Umma na Binafsi”*  ikiwa ni utekelezaji wa mpango mkakati wa kuunga mkono jitihada za Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania za kukuza na  kutangaza Utalii wa nchi yetu.

Aidha TAWA imetumia maonesho hayo kunadi fursa mbalimbali za utalii na uwekezaji zilizosheheni katika taasisi hiyo ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya uhifadhi kwa maelfu ya wananchi waliohudhuria katika maonesho hayo.

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram