162 views 35 secs 0 comments

TUMEENDELEA KUIMARISHA UDHIBITI NA KUKUZA MATUMIZI SALAMA YA TEKNOLOJIA YA NYUKLIA

In KITAIFA
May 07, 2024

JIJINI DODOMA

Adolf Mkenda alivyowasili Bungeni jijini Dodoma tayari kuwasilisha Bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

Bajeti ya Wizara ya Elimu kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 ina kauli mbiu inayosema ‘Elimu ujuzi ndio mwelekeo’ ikiwa na maana msisitizo na mkazo katika mitaala yetu utajikita zaidi katika kuhakikisha wahitimu wanakuwa ujuzi utakaowawezesha kujiajiri na kuajiri wengine.



โ€Serikali imeendelea kuimarisha udhibiti na kukuza matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia kwa kutekeleza yafuatayo:
imesajili vituo vipya 43 vya Mionzi ayonishi na kufikisha jumla ya vituo vya mionzi 1,386 vilivyosajiliwa na vituo vipya 42 vya mionzi isiyoayonishi na kufikisha jumla ya vituo vya mionzi isiyoayonishi 409 vilivyosajiliwa.

Aidha, Serikali imesajili vyanzo vipya 36 vya mionzi na kufikia jumla ya vyanzo vya mionzi 1,647 vilivyosajiliwa

Serikali imetoa leseni 633 za kumiliki na kutumia vyanzo vya mionzi, uingizaji nchini wa vyanzo vya mionzi 95, utoaji nje ya nchi wa vyanzo vya mionzi 13 na safirishaji wa vyanzo vya mionzi ndani ya nchi 47;
imepima viwango vya mionzi kwa wafanyakazi 1,980 wanaofanya kazi katika vyanzo vya mionzi katika vituo 429. Aidha, viwango vya mfiduo vilivyopokelewa katika miezi mitatu mfululizo vilianzia 0.1 hadi 3.2 millisievert (mSv), ambavyo viko ndani ya ukomo unaokubalika wa udhibiti. Prof Adolf Mkenda, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia

/ Published posts: 1480

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram