314 views 24 secs 0 comments

MRADI WA BBT KUTEKELEZWA KATIKA HALMASHAURI 100 NCHINI

In BIASHARA, KITAIFA
May 02, 2024

JIJINI DODOMA

Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb) akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara ya Kilimo kwa Mwaka 2024/2025, amesema wizara yake itaendelea kuwezesha upatikanaji wa ajira zenye staha na ushiriki wa vijana na wanawake kwenye kilimo kupitia utekelezaji wa Programu ya Jenga Kesho Iliyo Bora (Building a Better Tommorrow – BBT).

“Wizara itaendelea kutekeleza mradi wa mashamba makubwa ya Chinangali, Chunya, Singida na Ndogowe kwa kujenga mabwawa na kuchimba visima kwenye mashamba ya BBT jumla ya hekta 186,086. Vilevile, Wizara itaanza kutekeleza mradi wa BBT katika halmashauri 100 zitakazotenga maeneo yenye ukubwa wa hekta 200 kwa kila halmashauri na kujenga miundombinu ya umwagiliaji katika maeneo hayo,” amesema Mhe. Bashe.

Prrogramu hiyo inatekelezwa kupitia miradi mikuu minne ambayo ni kuwezesha upatikanaji wa ardhi ya kilimo na uanzishaji wa mashamba makubwa ya pamoja (Block farms) na umilikishaji wa ardhi, kuwezesha upatikanaji wa mitaji kwa vijana na wanawake (BBT – Mitaji), kuimarisha Huduma za Ugani (BBT – Ugani) na kuwezesha upatikanaji wa miundombinu ya umwagiliaji kwa wakulima wadogo (BBT – Visima).

/ Published posts: 1487

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram