256 views 55 secs 0 comments

TMDA YATOA UFAFANUZI WA DAWA YA XSONE YA MACHO KUWA HAIJAKIDHI MATOKEA KWA KUTUMIKA

In KITAIFA
February 27, 2024

Na Madina Mohammed

Mamlaka ya Dawa na vifaa tiba TMDA inawataarifu wananchi kuwa Kuna dawa aina ya XSONE ya macho inayotengenezwa na kiwanda Cha Abacus Paranteral Drugs Ltd (APDL) Kampala,Uganda dawa hiyo imebainika kutokidhi vigezo vya ubora ambayo ni matokeo DUNI.

Imethibitika kuwa Kwa dawa hizo kuwa DUNI Kwa kuwa yameonesha kuwa na vipande vidogo vidogo vya rangi ya kahawia (Brown) sehemu ya Chini ya kifungashio (Chupa) Tofauti na muonekano wa dawa hiyo ambayo ni ya kimiminika kisicho na rangi yoyote
“Sterile aqueous,Clear, Colorless solution”.

Kutokana na kubainika Kwa matoleo hayo mawili (2) ya dawa DUNI TMDA imeweza kutoa maelekezo Kwa wananchi


        **1wananchi wanaelekwaza kuangalia Kwa makini lebo Ili kutambua nambari za matoleo ya dawa tajwa na endapo wataona namba za matoleo hayo wasitumie dawa hizo Ili kuepusha madhara yanayoweza kutokea

      **2wauzaji wa dawa( jumla na rejareja) wanaelekezwa kutambua matoleo hayo na endapo watayabaini wasitishe.usambazaji na uuzaji wa dawa hizo na kurejesha matoleo hayo walikonunua.

     **3vituo vya kutolea huduma za Afya na hospital (binafsi na umma) wayabainishe na kuyatenga matoleo hayo na kusimamisha matumizi yake na Kisha kuyarejesha Kwa Usambazaji wake.

TMDA imeendelea kusema kuwa kufuatilia ubora wa matoleo mengine ya dawa hii na hivyo inawaomba wananchi kuendelea kutoa taarifa Katika ofisi za TMDA nchini ikiwa watabaini uwepo wa dawa inayodhaniwa kuwa DUNI au bandia Katika soko lao Ili kuweza kuzuia madhara yanayoweza kusababishwa na utumiaji wa dawa hizo.

/ Published posts: 1480

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram