143 views 2 mins 0 comments

KADOGOSA:UJENZI WA SGR YAFIKIA TRILION 23.3 MIAKA MITATU YA RAIS SAMIA

In KITAIFA
March 25, 2024

Na Mwandishi Wetu DAR ES SALAAM

MKURUGENZI wa shirika la Reli nchini (TRC) Masanja Kadogosa amesema Ujenzi wa Miundo mbinu ya Reli unatarajia kufikia takribani trion 23.3 ambapo tayari shilingi trioni 10 zimeshalipwa kutekeleza Mradi huo wa kimkakati.

Akizungumza Katika Mkutano wa waandishi wa Habari na wahariri wa vyombo vya habari nchini jijini Dar es Salaam Masanja kadogosa amesema kuwa zaidi ya Asilimia 70 ya Bajeti ya serikali imewekezwa katika ujenzi wa Ujenzi wa Reli ya Umeme (SGR) ambapo Endapo Reli hiyo itapunguza kero ya uondoaji wa Mizigo kwenda kwenye Bandari kwa kutumia Barabara.



“Wazo la kujenga Reli ya SGR lilianzia Awamu ya tatu ya Rais Hayati Benjamin Mkapa,likaanza kutekelezwa na Awamu yatano na kuendelezwa na Awamu ya Sita ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan”Alisema Mkurugenzi wa Shirika la Reli nchini Masanja kadogosa.

Mkurugenzi Kadogosa aliongeza kuwa katika Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita tayari ameshaanza kujenga reli hiyo Kutoka Uvinza hadi Msongati.



Alisisitiza kuwa Wajerumani walikuwa na wazo la kujenga Reli ya (SGR) lakini leo Rais wa Jamuhuri wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan ameweza kuziunganisha nchi za Afrika Mashariki.

“Tunategemea hadi kufikia March28 Mwakahuu kupokea vichwa 5vya treni vilivyo chongoka”Alibainisha Masanja Kadogosa.



Kadogosa Aliongeza kuwa tayari Serikali imeshaingia mkataba wa Ujenzi wa Reli ya (SGR) Tabora hadi Isaka n Benki ya Dunia .
Aliwaambia Waandishi wa Habari kuwa ujenzi wa Reli ya SGR kutoka Dar hadi Makotopola tayari Umeshafikia Asilimia 97.

” Kwa Mwaka fedha 2024/25 tunarajia kuanza wa Ujenzi wa SGR katika Mikoa ya Tanga ,Moshi na Arusha”Alibaisha Mkurugenzi Kadogosa .



Kwa Upande wake Mkuu wa Kitengo cha Habari wa Shirika hilo,Jamila Omar aliwaambia waandishi wa Habari kuwa lengo la Mkutano wa waandishi wa Habari na wahariri nikujenga uelewa kwa waandishi wa habari juu ya Mradi huo wa kimkakati.

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram