235 views 25 secs 0 comments

WATUMISHI WANAWAKE GST WAADHIMISHA SIKU YAO DUNIANI

In KITAIFA
March 08, 2024



*Waziri Gwajima atoa wito kwa Wanawake*

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, ametoa wito kwa Wanawake kufanya kazi kwa bidii na weledi kwa kuwa wanauwezo wa kufanya kazi nyingi  kwa umakini na kwa uaminifu mkubwa.

Dkt. Gwajima ameyasema hayo leo Machi 8, 2024 katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kilichofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Chinangali II iliyopo Wilaya ya Chamwino jijini Dodoma.

“Mwanamke ni Mama pia ni Kiongozi na ni mshauri mzuri katika jamii hivyo ni wasihi wanawake wenzangu tuendelea kuchapa kazi bila woga na tusichague  kazi pia tusijihisi kwamba hatuwezi kufanya kazi fulani,” amesema Dkt. Gwajima.

Kwa Upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Uendeshaji wa GST, Neema Muhagama, amewataka wanawake wa Taasisi hiyo kuendelea kujitokeza kufanya kazi kwa bidii kwa lengo la kuongeza mchango wa wanawake kwenye maendeleo ya Taifa.

Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Kitaifa yanafanyika jijini Dodoma ambayo yamebebwa na Kauli mbiu isemayo *”Wekeza Kwa Wanawake Kuharakisha Maendeleo Ya Taifa na Ustawi wa Jamii”*.

/ Published posts: 1883

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram