Na Madina Mohammed
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Azan Zungu amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo kusitisha zoezi la Mgambo kuwakamata Wafanyabiashara waliopo Jimboni humo badala yake wawaache wanfanye Biashara zao Kwa amani na utulivu.
Naibu Spika huyo ameyasema hayo mara baada ya kukutana na Wafanya Biashara wa Soko la Boma liliopo Wilayani humo Jijini Dar es salaam ambapo amesema nia ya Rais Dr Samia Suluhu Hassani ni kuajali na kuwasiliza Watanzania waishi kwenye mazingira ya amani na upendo.
Hata hivyo Zungu amemtaka Diwani wa kata ya Ilala Saady Kimji aunde Umoja wa Wafanyabiashara Wanawake waliopo sokoni hapo kwani Umoja huo utawawezesha kuwakomboa kiuchumi.
Pia amewataka Wafanyabiashara Wanaume kuacha kutumia lugha chafu Kwa Wafanyabiashara Wanawake ili kuepukana na udhalilishaji wa kijinsia.
Halmashauri ya Wilaya ya Ilala imetenga zaidi ya Bilioni ishirini Kwa ajili ya Ujenzi wa masoko ya kisasa katika Wilaya hio.
Ameyabainisha hayo Mkuu wa Wilaya hiyo Edward Mpogolo katika Mkutano uliowakitanisha Wafanyabiashara wa Soko la Boma liliopo Wilayani humo Jijini Dar es salaam ambapo amesema nia ya Serikali ni kuhakikisha inajenga Soko linaloendana na mazingira ya Jiji hilo.
Pia amewahakikishia Wafanyabiashara hao zaidi ya elfu nane watafanya Biashara ndani ya soko hilo pindi ujenzi utakapokamilika ili waweze kufanya Biashara zao katika mazingira salama.
Wakati huo huo mpogolo amewataka Wafanyabiashara Wanawake waunde Umoja ili Serikali iweze kuwatatulia changamoto zao.