Atangaza fursa katika sekta tano tofauti
Atangaza amani na kuimarika kwa kidiplomasia na kisiasa nchini
Na mwandishi wetu
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan baada ya kumaliza ziara yake nchi ya VATICAN , sasa atia timu Norway kwa ziara ya Kitaifa katika hatua za kuboresha mahusiano baina ya Tanzania na Norway.
Rais Samia amepokelewa na Mfalme Harald V wa Norway akiwa kama muenyeji wake na kufikishwa katika Kasri la Kifalme Jijini Oslo kwa ajili ya ziara yake ya Kitaifa.
Vile vile Rais Samia amefanikiwa kuzungumza na Wawekezaji wa Norway na kufungua milango ya fursa ya Uwekezaji huku akiwakaribisha kuwekeza hususani sekta za Kilimo,Nishati,Mafuta na Gesi,Miundombinu na Usafirishaji.Katika hatua nyingine Rais Samia awabainishia uwepo wa amani na utulivu wa kisiasa nchini Tanzania.