Na Mwandishi Wetu
Katiba wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi, Itikadi , Uenezi na Mafunzo Ndg. Paula Makonda akutana na Wajumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Dsm na Wilaya ya Kinondoni pamoja na Viongozi wengine mbalimbali kutoka Wilaya zingine 4 zinazounda jumla ya Wilaya 5 Mkoani Dsm, leo tarehe 19 Januari, 2024.
Akiwa hapo, amepokea taarifa ya kazi ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya Mkoa wa DSM na Wilaya ya Kinondoni ambazo zimempongeza kwa kuwa na ziara ambazo ni mbinu na chachu ya kuongeza Wanachama, Wapenzi na Mashabiki wa CCM.
Pamoja na hilo, wametoa Pongezi ya kuwa mhasisi wa Ujenzi wa Ofisi za Chama Cha Mapinduzi za gorofa Mkoani DSM katika kila Wilaya.