243 views 2 mins 0 comments

MKURUGENZI WA BANDARI MRISHO,TPA TUNAJIVUNIA KUPOKEA MELI KUBWA YA WATALII

In KITAIFA
January 16, 2024

Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Mrisho Seleman Mrisho amesema kuwa wao kama bandari wanajivunia kupokea meli kubwa ya watalii kwakuwa matarajio yao ni kupokea meli kubwa zaidi ya hiyo kwani tayari wameshafanya maboresho kadhaa ikiwemo kuongeza kina cha maji na mengine tofauti na ilivyokuwa awali kabla ya maboresho.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Januari 16, 2024 baada ya kupokea meli hiyo inayoitwa Norwegian Dawn iliyokuja na watalii 2210 Mkurugenzi huyo wa Bandari ya Dar amesema ujio wa meli hiyo utaweka historia kwakuwa ina urefu wa mita 294 na kwamba ndiyo ndefu kupokelewa katika bandari hiyo.

โ€œMeli hii uwezo wake ni kubeba watalii au abiria ni 4700, lakini waliokuja kwenye meli hii ni watalii 2,210 na crew kama 111 wale wanaofanya kazi ndani ya meli. Lakini jambo kubwa la kujivunia ni kwamba kampeni ya Royal Tour inaendekea kuzaa matunda, hawa watalii walioshuka wanaelekea kwenye vivutio vingine hapa Tanzania. Lakini sisi kama bandari tunafurahi kama ambavyo nao wamefurahi, makapteni wetu mashuhri wameenda kuichukua hii meli kule nje na kuja nayo ndani kwa usalama wa hali ya juu sana,โ€ amesema Mrisho.

Aidha Mrisho amejivunia maboresho wanayoendelea kufanya katika bandari hiyo ikiwemo kuchimba kina pamoja na kurekebisha mlango ambayo yamewezesha meli hiyo kutia nanga hapo. โ€œNa sisi matarajio yetu ni kuhudumia meli zenye urefu wa mita 305, tunajivunia meli hii ni ndefu, kubwa na capacity yake pia ni kubwa, tutakaa nayo hapa, tutailinda na wao wamefurahia hakuna tukio lolote lililotokea. Ikitoka hapa itaenda Msumbuji,โ€ amesema Mrisho.

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram