215 views 45 secs 0 comments

USIUPOTEZE MWAKA HUU KWA NAMNA HII

In MAKALA
December 27, 2023

Tunakaribia kuumaliza mwaka huu na kuingia mwaka mpya 2024.

Mwaka huu ulikuwa na mipango na mawazo mazuri mengi.
Yako ambayo uliyafanyia kazi na ambayo hujayafanyia kazi.

Kila mwaka lazima ufanye kitu cha ushindi, usiache mwaka uishe bila kupata kitu cha ushindi.

“Kila mwaka unaopita ambao hujaharibu moja ya mawazo yako pendwa ni mwaka ambao umeupoteza”

Kama mwaka unapita na hujajaribu moja ya mawazo yako, unakuwa umeupoteza mwaka wako.

Usikubali mwaka upite bila kujaribu mawazo yako mapya.
Kuupoteza mwaka ni pale ambapo unaumaliza bila kujaribu mawazo yako pendwa uliyokuwa nayo.

Bado unayo nafasi ya kujaribu kile unachojua ili uone je kinafanya kazi au hakifanyi kazi.
Usiseme haifanyi kazi kama wewe mwenyewe hujaifanyia kazi.

Hatua ya kuchukua leo; nenda kafanyie kazi mawazo yako pendwa uliyokuwa nayo kabla mwaka huu haujaisha.

Kumbuka, Bilionea Charlie Munger aliwahi kunukuliwa akisema, “Kila mwaka unaopita ambao hujaharibu moja ya mawazo yako pendwa ni mwaka ambao umeupoteza”
Usikubali kupoteza mwaka wako.

MUHIMU;
Kama bado hujajiunga na kundi la wasapu la Mimi ni Mshindi jiunge leo kwani kuna maarifa mengi unayakosa ambayo sikushirikishi hapa.

Kujua ni maarifa gani hayo na jinsi ya kujiunga nitumie ujumbe wasapu kwa namba 0717101505. Kupata vitabu vizuri vya kujisomea kwa lugha ya kiswahili wasiliana kwamba namba 0717101505.

Rafiki Na Mwalimu Wako, Afisa Mhamasishaji Mkuu (CIO)Chief Inspiration Officer.

/ Published posts: 1491

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram