123 views 2 mins 0 comments

TPSF KUANDAA SEMINA KWA KUSHIRIKIANA NA WADAU TAWA NA MATAASISI YA BANK

In KITAIFA
December 07, 2023

Na Madina Mohammed

Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF )kwa Kushirikiana na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori( TAWA ) zimefanya Warsha kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wataalamu wa Sekta ya Benki pamoja na Mawasiliano ili kuweza kushirikiana kwa pamoja kudhibiti Maliasiri.

Akizungumza na Waandishi wa Habari kando ya Warsha hiyo iliyofanyika Desemba 7 ,2023 jijini Dar es salaam Mejeja Miradi wa Kuhifadhi Maliasili kwa ufadhili wa USAID Bw.Godfrey Mondi amesema kuwa mradi wa kuhifadhi Maliasiri unatekelezwa kwa muda wa miaka mitano.

Amesema kuwa kumekuwepo na biashara haramu ya Wanyamapori,hivyo sasa ni wakati wa taasisi za serikali na sekta binafsi kushirikiana kwa pamoja ili kuwezesha kutunza rasilimari zilizopo kwa ajili ya vizazi vilivyopo navijavyo.

” Leo TPSF tumeshirikiana na TAWA kufanya semina hii kwa washiriki wa sekta ya benki na taasisi za Mawasiliano kwani hawa ni wadau muhimu ambao tunashirikiana nao katika kupambana na hali ya ujangili,mradi huu wa kuhifadhi Maliasiri unafanyika kwa muda wa miaka mitano na umefadhiliwa na wenzetu wa USAID”. amesema


Kwa upande wake afisa Wanyamapori kutoka TAWA ,Dolorosa Maricky amesema kwamba kwa sasa vitendo vya ujangili vimepungua nakwamba serikali inashirikiana vyema na sekta binafsi kuhakikisha hali ya ujangili isiendelee kujitokeza pamoja na kulinda Maliasiri.

” Lazima kuwepo na ushirikiano kati ya serikali na sekta binafsi ,hivyo warsha kama hizi zinasaidia kuleta umoja kati ya serikali na Sekta binafsi katika kuhakikisha tunapambana na ujangili” amesema

Nakuingeza kuwa taasisi za kifedha kama benki pamoja na taasisi za Mawasiliano ni wadau muhimu sana katika kuhakikisha tunafanikiwa kutunza Maliasiri hizi,hivyo tunaendelea kutoa mafunzo wadau wenzetu ili tushirikiane pamoja katika kuhifadhi maliasir hizi.

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram