94 views 3 mins 0 comments

GWAJIMA:MUSITUMIE KAUSHA DAMU MUTAKAUKA DAMU

In BIASHARA
September 12, 2023

Wizara ya maendeleo ya jamii Jinsia na makundi maarum ambayo imetenga kiasi kidogo Cha fedha Kwa ajili ya maendeleo ya wanawake WDF ambayo inaleta muongozo wa Asilimia kumi unaoboreshwa na unaungana na mwongozo wa mfumo wa wanawake ambalo lengo ni kuondoa wizara ambazo zinazofatilia mtu mmoja mmoja zipite Katika mabank na wapate mafunzo na elimu Ili mahesabu Yao yakawe mazuri

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ameweza kuwaweka wanawake kuwa pamoja kwenye majukwaa Yao na wazungumze lugha Yao na wakute kwenye majukwaa Yao kama madarasa

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Leo Jumatatu 11 September 2023 waziri ya maendeleo ya jamii Jinsia na makundi maarum Dorothy Gwajima amesema Huu ni mkakati imara ambao ameuweka Rais Samia Suluhu Hassan ambalo tunalo jukwaa la kitaifa na jukwaa la MKOA na majukwaa ya wilaya

“Dkt.Rais Samia Suluhu Hassan ameazisha haya majukwaa anataka watu wapate taarifa na waachane na mikopo hii ya kausha damu ambapo Wanakosa taarifa ya sahihi ya kitu Gani na wakipate wapi na kwanini wasiende imbeju kutoka CRDB” amesema Gwajima

Serikali inafanyia kazi mpango WA taifa WA kusimamia maendeleo ngazi ya msingi 2023 tunakwenda mpka 2026 kutakuwa na hamsha hamsha pamoja na maafisa maendeleo jamii wetu kuwaeleza wananchi Ili wanapoelewa somo wajiunge Katika vikundi na waanze kuzipata hizo FURSA ila upo Utekelezaji wa mfumo jumuishi wa kidigitali na usajili wa vitambulisho wa wafanyabiashara ndogo ndogo


“Kwa wamachinga na mfumo huo unaenda kuzinduliwa tukiuzindua inabidi mujiunge na mupate vitambulisho vya kidigitali na utakuwa unasomeka Katika mabank yote na taasisi zote na kujua FURSA zote na ukienda kulipa utaaminika”ameongeza Gwajima

Aidha ameeleza kuwa Kuna juhudi zengine zimefanyika ya kuanzisha program ya Jinsia anaweza inayolenga kuwawezesha.wanawake.kiuchumi na kushiriki nafasi za uongozi na program hiyo imegharimi pesa TAKRIBANI MILIONI 7 .5

Nae mkuu wa wilaya ya Ilala Endward Mpogolo amesema Serikali Kwa kushirikiana na RAIS Samia Suluhu wameona FURSA muhimu Kwa kuwawezesha wajawasiriamali na Kwa niamba ya serikali ndio iliyowafanya kuwaahidi wajawasiriamali hawa kujiwezesha Kwa kujikamua Kupitia mifuko ya jamii na account ya imbeju KUTOKA CRDB

Aidha mkuu wa wilaya amesema watajitahidi kuwapatia masoko na jitihada hizo zitakuwa sambamba na mhe.rais

“Mpka mwezi juni 2023 imepatikana mikopo Zaidi ya BILIONI 27 Kwa mikopo hiyo Kwa Zaidi ya vikundi 2063 vimenufaika lakini vikundi hivyo vimeweza kufanya marejesho Zaidi ya asilimia 10 Zaidi ya BILIONI 17.9″amesema Mpogolo

Madina Mohammed

/ Published posts: 1215

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram