260 views 17 secs 0 comments

KAJALA AJIBU SHUTUMA ZA HARMONIZE KUUZA RANGE

In BURUDANI, KITAIFA
August 09, 2023

Mwigizaji staa kajala masanja amefunguka kwenye Mkutano wake na waandishi wa habari kuhusu yanayoendelea mtandaoni kumuhusu yeye na EX wake Harmonize ambapo amekiri kwamba ni kweli miezi miwili kabla hawajaachana na Harmonize alikuwa anachukua asilimia 10 kutoka kwenye kila hela aliyokuwa akiingiza Harmonize

Akiongea Leo jijini Dar es salaam wakati akigewa Dili la ubalozi wa Pedi,kajala pia amethibitisha madai ya Harmonize kumpa msaada baba yake mzazi ambapo amesema ni kweli lakini amekanusha madai kwamba ameuza Range aliyopewa na Harmo.

“Gari Mimi sijauza, gari IPO ila napenda tu kutembelea gari ya Paula Ile Toyota kwani nakuwaga nayo nipo free sipendi kutembelea Range kwani range sipendagi watu wakiniona na kuniitaita”. Amesema Kajala

Aidha kuhusu password za benki za akaunti za Harmonize amesema sio yeye tu Vijana wote wa konde gang wanazo na kuhusu ishu ya Anjela kuondoka konde gang amesema hata yeye ameshangaa kwani aliwai kumfuata Harmonize na kumuomba amuachie hata gari kwani ni mgonjwa

Madina Mohammed

/ Published posts: 1215

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram