Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Bernard Kamungo anayecheza FC Dallas ya Marekani, alfajiri ya leo alikuwa uwanjani kucheza dhidi ya Inter Miami inayochezewa na Lionel Messi katika mchezo wa Kombe la Ligi (North & Central America League Cup).
Katika mchezo huo ambao uliongezeka mvuto kutokana na uwepo wa Lionel Messi dakika 90 zilimalizika kwa sare ya 4-4 huku Kamungo akifunga goli la pili kati ya manne ya FC Dallas.
Lionel Messi alikuwa shujaa wa timu hiyo baada ya kuisaidia kufunga magoli mawili wakiwa nyuma na kufanya mchezo umalizike timu ya Messi (Inter Miami) kupata ushindi wa penati 5-3, huku Kamungo akiandika historia ya kuwa Mtanzania wa kwanza kuwahi kucheza dhidi ya Lionel Messi.