
Wanasheria wazalendo wamesema Moja ya sera ni uwekezaji Katika sekta ya kiuchumi na kijamii Katika kutekeleza sera za uwekezaji serikalini pia Ina mamlaka ya kuingia makubaliano na mwekezaji wa ndani au nje ya nchi kuendeleza na kuboresha rasilimali tulizonazo kwa manufaa ya jamii na taifa kwa ujumla.
Wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Leo ijumaa 04 august 2023 mwenyekiti wa mawakili wazalendo Juma Nassoro Amesema serikali imeweka utaratibu wa kutambua mwenye nia na uwezo wa kuwekeza Katika rasilimali tulizozikuwa nazo Nchini kupitia wataalam wake na kwa kuzingatia taarifa ilizo nazo kuhusu mwekezaji kuhusika na manufaa tunayotarajia kuyapata kama Taifa.
“makubaliano tunayoyazungumzia ni sehemu tu ya mikataba mingi ambayo serikali imeingia na wawekezaji kwa ajili ya uendelezaji na uboreshaji wa rasilimali zetu katika sekta mbalimbali kwa maslahi na manufaa ya kiuchumi kwa ustawi wa jamii na taifa kwa ujumla”.Alisema Nassoro
Alibainisha kuwa mahakama na bunge ni kuisaidia serikali kufanikisha Utekelezaji wa jukumu hili zito na sio kuukwamisha Katika makubaliano haya serikali imefanya jukumu lake kwa kutekeleza mamlaka iliyopewa Kwa mujibu wa ratiba,sheria na desturi zinazotawala
“Baada ya kufanya majadiliano, makubaliano yaliandaliwa na kusainiwa ibara ya 31 ya makubaliano inahitaji makubaliano hayo kuridhiwa na hapa kwetu Wenye mamlaka ya kuridhia ni bunge chini ya Ibara ya 63(3)(c) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,bunge ndicho chombo ambacho kina wawakilishi wa wananchi”. Ameongeza Nassoro
Aidha wamesema serikali imetekeleza wajibu wake na itaendelea kusimamia Utekelezaji wake kwa mujibu wa sheria na kanuni za nchi na tunaunga mkono juhudi hizo za serikali za kutafuta wawekezaji kutekeleza sera na Sheria za nchi
Madina Mohammed