Ibrahimu Traore ni Afisa wa jeshi la Burkina Faso ambaye kwasasa ni Rais wa nchi hiyo baada ya kufanyika kwa mapinduzi ya kijeshi yaliyomwondoa madarakani rais Paul-Henri Sandaogo Septemba 30, 2022
Traore alizaliwa mwaka 1988 katika mji wa Bondokuy, Burkina Faso kwa Sasa ana umri wa miaka 35 kitu kunacho pelekea kuwa Rais mwenye umri mdogo zaidi barani Afrika.
Siku za hivi karibuni amekuwa miongoni mwa viongozi barani Afrika wanaozungumziwa zaidi kwenye vyombo mbalimbali vya habari duniani huku wakimfananisha na kiongozi wa zamani wa nchi hiyo Thomas Isdorรฉ Sankara kutokana na misimamo yake mikali dhidi ya nchi za magharibi zinazonyonya maliasili za bara la Afrika.
Tangu Kapteni Ibrahim Traorรฉ aingie madarakani amejaribu kuitenga nchi yake na Ufaransa na kuwa karibu na nchi zisizo za magharibi. Traorรฉ amewahi kutunukiwa nishani ya BRICS (Muungano unao jumuisha nchi za Brazil, Russia, India, China na South Africa).