454 views 2 mins 0 comments

JESHI LA POLISI:WAMKAMATA MTUHUMIWA ALIETUKANA VIONGOZI WA SERIKALI

In KITAIFA
August 01, 2023

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemkamata na linamuhoji kwa kina Selemani Agai Gaya mwenye umri 18) mkazi wa Kigamboni, kwa tuhuma za kutoa lugha ya matusi mtandaoni dhidi ya Viongozi wakuu wa Serikali Tanzania kwa kutumia mitandao wa kijamii.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Leo jumanne 01 Agosti 2023 Kamanda wa polisi Kanda maarum ya Dar es salaam Murilo jumanne murilo amesema Mtuhumiwa huyo amekamatwa Julai 29, 2023, na wenzake ambao wamekuwa wakitengeneza maudhui za mtandaoni (video) na kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii zenye kuwatukana na kuwafedhehesha viongozi wakuu wa Serikali katika akaunti zao za Tiktok. Mtuhumiwa huyo atafikishwa Mahakamani.

Aidha Jeshi la Polisi linatoa onyo kali kwa mtu/ watu wanaotoa lugha za matusi na fedheha kwa Viongozi wa Serikali kwa njia ya mtandao na njia nyingine yoyote, kuwa Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na mamlaka nyingine za kisheria limejipanga kuwafuatilia na kuwakamata, kuwahoji kwa kina kuhakikisha wanafikishwa haraka kwenye nyombo vya sheria.

Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Julai 31, 2023 limewakamata watuhumiwa saba akiwemo Amani Kipolo mkazi wa Vingunguti kwa tuhuma za kumshambulia na kusababishia kifo Hadija Hamisi na kuwajeruhi watu wengine nane (8).

“Watuhumiwa hao wakiwa na wenzao wakiwa kwenye kundi waliwashambulia wananchi mtaani maeneo ya Vingunguti kwa lengo la kulipiza kisasi wakati wakitoka kuzika mwenzao aliyefahamika kwa jina la Nurdin Bwino”. Amesema Murilo

Hata hivyo awali Murilo amesema marehemu huyo Nurdin Bwino aliuwa kwa kushambuliwa na wananchi alipokuwa na wenzake sita wakiwa na visu na vifaa mbalimbali vya kuvunjia alipojaribu kuvunja nyumba moja usiku wa Julai 30, 2023.

Madina Mohammed

/ Published posts: 1883

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram