209 views 3 mins 0 comments

JERRY SILAA:AWASHANGAA WANASHERIA WANAOPOTOSHA TAFSRI YA VIPENGELE VYA MKATABA

In KITAIFA
July 12, 2023

Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya uwekezaji wa mitaji ya Umma (PIC) ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la ukonga Jerry Silaa amesema nchi yetu inakatiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inayotoa mamlaka Kwa kila aliepewa mamlaka na katiba,katiba hiyo imeazimishwa na mamlaka lakini vile vile mamlaka hayo wakitumia Demokrasia Kwa kupata viongozi kwa kuwachagua wabunge na Mimi nimechaguliwa mwakan 2020 Kwa kupata kula 126000 pia wanamchagua na Rais na kuunda serikali na kila mmoja anaingia Katika majukumu yake.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam Leo ( jumatano 12 julai 2023 ) Jerry slaa amesema Kwa kuwa swala hili limekuja Bungeni na kanuni Ile ya mia na 7 ilikuja kwenye kamati ya kunuku ya kamati ya pamoja na aina ya kamati ya Umma na kamati ya miundo mbinu

Jerry Silaa amesema amesema Tarehe 16 iliingia Bungeni na kamati yetu ilitoa taarifa na bunge likajadili na hatimae likaridhiwa baada ya kuridhiwa ni wajibu wa serikali kuendelea na michakato mingine ya utendaji kama ilivyoainishwa na katiba.

“Nimeona Kuna watu wachache walioamua kupotosha Kwa sababu wanaozijua wao sababu hizo nitazielezea badae Kwa kuwapotosha Umma lakini wakishawapotosha wapo watanzania wengi Wenye Nia njema ambao nao wanasikia yanayosemwa ilikuwa tengenezea taharuki”.

“nimeona upotoshaji unazidi kuwa mkubwa na watanzania wanaitaji majibu na pia vile vile ni wajibu wangu kutoa majibu Kwa yale ninayoyafahamu”. Amesema Jerry silaa

Aidha Silaa ametumia fursa hiyo kuwahatadharisha wananchi kuwa Kuna watu wanatumika Kwa maslahi wanaowajua wao wenyewe Kwa jitihada kubwa za kumuondoa kwenye reli Rais wetu Dkt.Samia Suluhu Hassan ambae kwaa wakati wote amekuwa akifanya kazi kubwa ya kujenga uchumi wa taifa letu na kutekeleza ilani ya uchaguzi.

“ukiwasikiliza wengi mtu anaweza kuongea Kwa dakika 15 lakini hakuna sehemu yoyote anafika kuzungumzia Yale makubaliano yenyewe yaliyoingia kati ya serikali yetu na serikali ya Dubai na wanafanya hivyo Kwa makusudi Kwa sababu yapo maneno mengi unaweza kuongea na ukatengeneza sintofahamu na taharuki”. Amesisitiza Silaa

Hata hivyo amesema zipo hoja za kisheria ambazo na zenyewe ninasikitishwa na baadhi ya wanasheria kuzijadili Katika mlengo ambao aidha hawazifahamu au wanafanya makusudi Kwa mfano IGA ni makubaliano ya kimataifa.

IGA ukiisoma hakuna eneo lolote la bandari inaenda kubinafsishwa IGA inaenda kujenga msingi wa kwenda kuingia kwenye mkataba WA uendeshaji,Swali ni je hii ni mara ya kwanza? Leo ukienda uwanja wa ndege WA Mwl Nyerere unamilikiwa na serikali kupitia mamlaka ya viwanja vya ndege lakini ukienda kuangalia opereshani za uwanja zinafanywa na sekta binafsi.

Madina Mohammed

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram