Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama amewataka watu wote ambao wanania mbaya ya kuichafua nchi yetu wanahitajika kupambana nao bila ya kumuogopa mtu yeyote na pia bila ya kumuonea haya mtu yeyote yule.
Aidha amewataka Viongozi mbalimbali wakiwemo wabunge,pia wameshauriwa kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake anazofanya katika kuhakikisha uchumi wa nchi unakuwa.
Akizungumza mapema leo,Julai 6, 2023, Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama, amesema kuwa Wabunge pamoja na viongozi wengine wanapaswa kuwa imara katika kupeperusha sera nzuri za Tanzania, na kwamba, hawapaswi kubaki nyuma katika kuunga mkono jitihada za Mheshimiwa Rais.
โWatu wote ambao wenye nia mbaya na nchi yetu, lazima tupambane nao bila kuwaogopa wala kuwaonea haya. Nchi yetu ni ya kila mtamzania, na ana haki ya kupambana kuhakikisha Amani, Utulivu na mshikamano tulionao unaendelea kuwepo.
โRais anafanya kazi kubwa sana, mambo mengi yalikuwa hayaendi, lakini sasa mambo yanaenda vizuri sana, wawekezaji wakubwa, wadogo na wa kati wanakuja kuwekeza nchini kwetu, haya yote ni matunda yatokanayo na yeye kutembelea kwenye Nchi mbalimbali za kigeni kuunganisha Biashara ili kukuza uchumi wa nchiโ amesema.
Hata hivyo Msama amesema tutahakikisha nchi yetu inaendelea kukiuza uchumi na nchi yetu ni nchi ya kila mtanzania anahaki ya kupambana kuhakikisha kuwa na amani na utulivu tuliokuwa nao na tunaendelea kuwa nao.
Pia amemshukuru Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan kuwa anafanyia kazi kubwa sana Kwa ajili ya kuinua uchumi wa nchi yetu,Mhe.Rais anafanya kazi kubwa sana analeta wawekezaji wengi sana tukumbuke kuwa uchumi wa nchi yetu ulikuwa umeyumba ila Sasa munaona uchumi unakuja Kwa Kasi sana.
Madina Mohammed