337 views 24 secs 0 comments

WAZIRI MKUU APOKEA TAARIFA YA WAFANYA BIASHARA KARIAKOO

In KITAIFA
June 21, 2023

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Alhamisi, Juni 21, 2023 amepokea taarifa ya Kamati Maalum aliyoiunda kwa ajili ya kupitia, kuchambua na kutoa
mapendekezo ya kutatua changamoto za wafanyabiashara nchini.

Taarifa hiyo imekabidhiwa na Mwenyekiti wa kamati, Dkt. John Jingu ambaye pia ni Katibu Mkuu, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum.


Mkutano huo umehudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista
Mhagama, Waziri Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba, Waziri wa
Viwanda na Uwekezaji Ashatu Kijaji, Waziri wa Nchi OR – TAMISEMI, Angela
Kairuki, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Ahmad Chande, Makatibu Wakuu,
Makamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wanakamati na
wataalam kutoka sekta mbalimbali za masuala ya kodi, biashara na uwekezaji.


Akizungumza baada ya kupokea taarifa hiyo, Mheshimiwa Majaliwa amesema
Kamati hiyo imefanya kazi kubwa na imeleta majibu ambayo yatatatua
changamoto za wafanyabiashara nchini na ameahidi kuwa Serikali imepokea
taarifa hiyo na itayafanyia kazi mapendekezo na ushauri uliotolewa na kamati hiyo.


Kamati hiyo ambayo ilipewa siku 14, imefanya mapitio katika maeneo
mbalimbali ya kikodi, bandari, maeneo ya wafanyabiashara kwenye mikoa
mbalimbali nchini.

Madina Mohammed

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram