215 views 2 mins 0 comments

LIPUMBA:Alipua mkataba wa bandari asema bandari inahusu Tanzania

In KITAIFA
June 21, 2023


MWENYEKITI wa chama cha wananchi the civil United Front (Cuf) Prof Ibrahim Lipumba amekemea vikali kuhusisha suala la mkataba wa kampuni ya Dp world ya nchini Dubai na Bandari ya Dar es Salaam (TPA) kuwa suala hilo Halina uhusiano wa uzanzibari nakusisititiza kuwa suala hilo linalohusu nchi ya Tanzania.


Akizungumza na Waandishi wa habari kwenye ofisi za makao makuu za chama hicho mapema hii leo jijini Dar es Salaam Professa Lipumba amesema kuwa suala hilo ni Bandari ya Dar es Salaam kutoa zabuni ya uendeshaji wa bandari hiyo na kati ya kampuni ya Dp world ya Dubai na Bandari ya Dar es Salaam TPA .


“Kuna mtu anaweza kuwa na agenda yakutugawa unaweza kusikia Tabora itakuwa katika sehemu ya kusukuma tusingie kwenye kuigawa Tanzania “.Alisema Professa Lipumba.


Lipumba Alisema kuwa ikumbukwe kuwa Rais wa Tanzania ni Dk Samia Suhulu Hassani,Mkataba huu unakasoro za kisheria naunapozungumzia Bandari ni kati ya Tanzania bara na Tanzania visiwani.


Alisema kumekuwa nachangamoto yakisera ya ukusanyaji kodi nakubainisha kuwa Mapato yanayokusanywa nikidogo ukilinganishwa na pato la taifa.


“Hakuna tathimini ya kisera ya tozo katika mihamala ya simu katika bajeti iliyopita 2022/23.kodi ya saruji ya kiwango cha kg 50 itatozwa shilingi 1000”.Aliongeza Professa Lipumba.


Professa Lipumba Aliongeza kuwanivyema serikali kufanyia marekebisho ya sheria ya uwekezaji ilikuweza kukuza sekta hiyo nchini.
Aliongeza kuwa Nivyema wizara yafedha kuweza kutathimi mifumo ya kodi ili iwezekuwa rafiki.


“Tuwena dhahabu zakutosha ilikuwa nafedha zakigeni katika ununuzi wa bidhaa ilikuweza kupunguza mfumuko wa bei za bidhaa”Alisisitiza Prof Ibrahim Lipumba.

Madina Mohammed

/ Published posts: 1215

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram