208 views 2 mins 0 comments

Nchemba aishukuru bank ya standard chartered

In KITAIFA
June 20, 2023

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, akutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered anayesimamia nchi za Afrika na Mashariki ya Kati, Bw. Sunil Kaushal

Benki ya Standard Chartered ipo katika hatua za mwisho za utaratibu wa kupata fedha kwa ajili ya ujenzi wa vipande vilivyobakia vya reli ya kisasa kwa Kiwango cha Kimataifa (SGR) ikiwa ni pamoja na kipande cha Makotopora-Tabora, Tabora – Isaka, Isaka-Mwanza na kipande cha kuanzia Tabora hadi Kigoma.


Tanzania na Benki ya Standard Chartered, imekuwa na ushirikiano mzuri katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo ya reli ambayo inaendelea vizuri.

“Tumekuwa na majadiliano kuhusu vipande vya reli ambavyo taratibu za kupata fedha zilikuwa hazijakamilika kikiwemo kipande cha Makotopora-Tabora, Tabora – Isaka, Isaka-Mwanza na kipande cha kuanzia Tabora hadi Kigoma”, alisema Nchemba

Aidha Nchemba alimshukuru Mkurugenzi huyo na timu yake kwa ujumbe waliouleta ambao unaeleza kuwa Benki hiyo ipo kwenye hatua za mwisho za taratibu za kupata fedha kwa ajili ya vipande hivyo vya Reli

Reli ni miongoni mwa miradi ya kipaumbele katika Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan na mara zote amekuwa akiuliza upatikanaji wa fedha umefikia hatua gani

Nchemba Alisema kuwa kwa sasa anayofuraha kumpelekea ujumbe, Mhe. Rais kuwa upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa vipande hivyo umefikia hatua nzuri.

Hata hivyo ameipongeza timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango kwa kukamilisha masuala mbalimbali yaliyokuwa yamejitokeza likiwemo suala la mazingira ambalo limepatiwa ufumbuzi

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered anayesimamia nchi za Afrika na Mashariki ya Kati, Sunil Kaushal, alisema kuwa Tanzania inafanya juhudi kubwa katika kusimamia uchumi na pia inafursa nyingi za uwekezaji ikilinganishwa na nchi nyingi za Afrika zikiwemo za Afrika Mashariki na kwamba Benki yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuwezesha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa Reli ya Kisasa.

Madina Mohammed

/ Published posts: 1485

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram