316 views 55 secs 0 comments

Tanzania yapaa kimataifa,waziri mbarawa kuboresha barabara Kwa njia ya EPC-F

In KITAIFA
June 16, 2023

Serikali imesema kuwa Utekelezaji wa miradi Saba ya ujenzi wa barabara Kwa njia ya EPC-F haitalipiwa na wananchi watakaotumia baadhi ya wananchi wanavyodhani.

Akizungumza jijini Dodoma Waziri wa ujenzi na uchukuzi Professor Makame mbarawa wakati wa utiaji Saini wa miradi hiyo ambayo inatarajiwa kutekelezwa katika Kanda za kaskazini na kusini na kujengwa na makandarasi wanne(4)

“Tanzania Haina barabara za kulipia mpaka Sasa hivyo upotoshaji unaosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kulipia kwenye barabara hizi si sahihi kwani barabara hizi ni za kawaida ‘high way’ kama zilivyo barabara nyingine”Alisema mbarawa

Waziri mbarawa amesisitiza kuwa mradi huu ni wa kwanza na mkubwa kutekelezwa Nchini kwani utapita katika mikoa 13 na lengo likiwa ni kuboresha mtamdao wa barabara Nchini na kuongeza ufanisi katika sekta ya usafiri na usafirishaji ili kuchochea uzalishaji katika maeneo zinazopita barabara hizi na kuongeza Kasi ya ukuaji wa uchumi wa wananchi wa taifa Kwa ujumla.

“Barabara zitakazojengwa zitapita katika mikoa ya morogoro,Ruvuma,Arusha,Manyara,Dodoma,Tanga,Singida,Mbeya,Songwe,Lindi,Mtwara,Simiyu,na Iringa na hivyo zitarahisisha usafirishaji usafiri wa mazao ya misitu, Biashara, Chakula,Uvuvi,na Ufugaji malighafi za madini kama vile makaa ya mawe,Grafiti na Chuma”Akifafanua waziri mbarawa

Aidha mbarawa ametaja miradi itakayotekelezwa kuwa ni ujenzi wa barabara ya kidatu,ifakara-lupiro-malinyi-kilosa mpepo-londo-lumecha/songea(km 435.8) Barabara ya Arusha-kibaya-kongwa(453.42) Handeni-kiberashi-kijingu-njoro-Olboroti mrijo Nchini Dalai-chambala-chemba-kwa mtoro-singida(km 284.33) Igawa-songwe-tunduma(km 237.9) masasi-nachingwea-liwale(km175) karatu-mbulu-Hydom-sibitiriver-lalago-maswa(km339) na barabara ya mafuga-mtwango-mgololo(km 81)

/ Published posts: 1615

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram