90 views 14 secs 0 comments

Mabachela kazi IPO,kujisajili Kwa sh 200.000

In KITAIFA
June 16, 2023

Umewai kujua kwamba ili utambulike rasmi kisheria kwamba haupo katika mahusiano kindoa “single”unahitajika kuw a na cheti Cha serikali (Bachelor Spinster certificate)kinachotolewa na wakala wa usajili,ufilisi na udhamini (RITA)

Huduma hiyo ya utambuzi huo ambao happy awali ilikuwa ikitolewa Kwa gharama ya sh 100.000 Kwa Sasa itaanza kupatikana Kwa kiasi Cha sh.200.000 ifikapo julai mosi mwaka huu,na ili ni Kwa mujibu wa mapendekezo yaliyotolewa na wizara ya fedha na mipango ikiwa Bungeni litaridhia.

Mapendekezo hayo yametolewa Jana katika hotuba ya waziri wa fedha na mipango Dkt mwigulu Nchemba wakati Akiwasilisha Bajeti ya serikali ya mwaka 2023/24 Bungeni. Jijini Dodoma.

Katika kiambatanisho namba 11 Cha majedwali kimeonyesha namba ongezeko la asilimia 100 mpaka 1000 katika huduma mbalimbali ambazo hutolewa na wakala wa usajili, wa talaka umeongezeka kutoka sh.20,000 mpaka kufikia sh 40,000.

Takwimu za RITA za mwaka 2020 zinaonesha kuwa wakala ulisajili talaka 511 Tanzania nzima kati ya hizo 221 kutoka Dar es salaam pekee.

/ Published posts: 1214

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram