
Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA
MMILIKI wa Kampuni ya Rohama 333, Mhandisi Owden Mwalyambi amemuangukia Rais Samia Suluhu Hassan kumuomba msaada ili aweze kulipwa malipo yake anayodai kufanyia kazi mradi wa serikali mkoani Rukwa bila kulipwa.
Mwalyambi ameeleza hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Ngome Social Hall, Wilaya ya Kinondoni Dar es salaam akimuomba Rais Samia aweze kusikia kilio chake ili haki iweze kutendeka juu yake.
Akieleza hayo amesema kuwa imani yake ni kuwa Rais Samia ni tais wa haki na analengo la kusaidia wananchi wake kupata haki kama wanavyostahili na kudhihilisha hilo ameanzisha hadi kampeni ya msaada wa kisheria ili kuweza kusaidia wananchi wake.
“Shida yangu ujumbe ufike kwa rais, kwa sababu usiku na mchana anatafuta mtu anayeonewa sasa mimi ninaamini habari hii ikifika kwake mimi hela zangu ntapata, ninaamini Makamu mwenyekiti wa chama ananguvu, Katibu Mkuu, nawaomba nifikishieni ujumbe kama ulivyo,” amesema Mwalyambi.
Aidha, akifafanua kuhusu changamoto iliyomfanya kumuangukia Rais Samia, Mwalyambi amesema miaka 13 iliyopita alisaini mkataba na serikali kwa ajili ya ujenzi wa barabara mkoani Rukwa na kudai kuwa alifanyia kazi mradi huo na kuukamilisha kwa asilimia 100.
Ameendelea kueleza kuwa wakati akiendelea na kazi ulitokea mvutano na kuambiwa kuwa alikuwa anadaiwa na serikali asilimia 20 ya kazi ambayo hajaikamilisha, ameeleza kuwa kwa upande wake alisema kama asilimia 20 wanasema haijakamilika aliomba alipwe asilimia 80 ya kazi aliyoifanya.
Mwalyambi amedai kuwa baada ya mvutano usiokuwa na mafanikio aliamua kupeleka kesi mahakamani na kukata rufaa mara kadhaa lakini juhudi hizo hazikuzaa matunda na kudai baadae aliamua kuiondoa kesi hiyo mahakamani kwa kukosa namna na kutokana na shinikizo na changamoto alizokuwa akipitia.
Amesema kuwa kutokana na hali ya madeni aliyokuwa nayo alikimbia na kwenda nchini Kenya kwenye kamni ya wakimbizi inayoitwa ‘Capital West’ kwa sababu aliambiwa hapo wanakaa watu walikubaliwa kwenda Ulaya lakini aliambiwa kutokana na juhudi za Rais Samia kuhakikisha watu wanapata haki akiamua kukimbia basi ni kumnyima haki rais ya kumsaidia.
Amesema anaamini kuwa Rais anamambo mengi lakini kila mahali anapokwenda anaambiwa anayeweza kumsaidia ni rais, akisitiza suala lake ni kuomba awese kulipwa fedha yake kwa sababu ameifanyia kazi na ili imsaidie kulipa madeni yanayomkabili.
“Mimi ninachotaka fedha zangu wanilipe madeni yanazidi sikuiba nimefanya kazi kwa mkono wangu,” amesema Mwalyambi.