
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko leo Aprili 26, amewasili mkoani Iringa kwa ziara ya kikazi ya siku moja.
Katika Uwanja wa Ndege wa Nduli, Dkt. Biteko amepokelewa na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa Iringa Mhe. Peter Serukamba
Akiwa mkoani humo anatarajiwa kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Sherehe za kuwekwa wakfu Askofu Mteule Romanus Elamu Mihali kuwa Askofu wa Jimbo la Kitume la Iringa.


