
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Ndg. Gerson Msigwa, Watendaji wa Wizara hiyo pamoja na Maafisa Utamaduni na Maafisa Maendeleo ya Michezo Tanzania, wameshiriki bonanza katika Uwanja wa Tanganyika Packers, Kawe jijini Dar es Salaam leo Aprili 26, 2025.
Bonanza hilo limehusisha michezo mbalimbali ikiwemo kufukuza kuku, kukimbia na magunia na mpira wa miguu uliohusisha mashabiki wa klabu za Simba na Yanga.
Timu ya Mashabiki wa Yanga SC imeshinda kwa mikwaju ya penati, baada ya kutoka sare ya 1-1 kwenye dakika 90.
Ushindi huo wa mashabiki wa Yanga umewawezesha kunyakua kitita cha shilingi milioni moja (1,000,000) ya goli la Mama.









