๐Ni kupitia ruzuku ya bei mitungi ya gesi ya kupikia
๐Gairo yahamasika na nishati safi
Wananchi Mkoani Morogoro wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuibeba ajenda ya nishati safi ya kupikia ili kukuza uchumi wa watazania.
Pongezi hizo zimetolewa na wananchi wa wilaya ya Gairo kwa wataalam wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wakati wakitoa elimu na kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia mkoani Morogoro.