9 views 2 mins 0 comments

WABUNGE WAITAKA WIZARA YA FEDHA IIPE FEDHA WIZARA YA TAMISEMI ITEKELEZE MAJUKUMU YAKE

In KITAIFA
April 22, 2025



Na Mwandishi wetu, Dodoma

WABUNGE mbalimbali wameipongeza Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa ufanisi wao ambao wamekuwa wakiufanya katika kuhakikisha miundombinu, elimu, afya na mambo mengine yanafanyika kwa ustadi mkubwa.

Akichangia bungeni bajeti ya TAMISEMI kwa mwaka wa fedha 2025/2026 Mbunge wa jimbo la Korogwe Vijijini Mhe Timotheo Mnzava amesema kuwa anakubaliana na kazi kubwa ambayo imekuwa ikifanywa na TARURA huku akisema kuwa wanmaiomba wizara ya fedha iwapelekee TAMISEMI, Tarura  fedha ili waweze kutatua changamoto zilizopo.

“Tunaipongeza serikali kwa kipindi cha miaka minne mitano tumefanya kazi kubwa sana na serikali imeleta fedha nyingi sana kuunga mkono ujengaji wa maboma ya madarasa  na zahanati” Amekaririwa Mnzava

Naye Mbunge wa Jimbo la Sengerema Mhe Hamis Tabasam amesema kuwa serikali za mitaa imebeba maslahi makubwa ya wananchi na kusema kuwa sengerema walikuwa wana matatizo ya shule za sekondari, shule za msingi Barabara na hata huduma za afya.

“Lakini katika kipindi hiki cha miaka minne Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa kuhakikisha huduma za kijamii katika nchi hii zinaboreshwa kwa kiwango kikubwa”amesema.

Jambo hili linatutolea hofu kwa sisi wabunge hakuna mbunge ambaye atakuwa na mashaka yakutokuchaguliwa jimboni kwake labda kama anahali mbaya damu zimechafuka tu maana kila kitu kipo vizuri kwa sasa.

Hata hivyo naye Mbunge wa jimbo la Nyamagana Mhe Stansilaus Mabula amesema kuwa kumekuwa na utulivu wa kiwango cha hali ya juu wizara ya TAMISEMI tangu alipoteuliwa Waziri Mhe Mohammed Mchengerwa .

Tunaposema hakuna kilichosimama hakika tunamaanisha kwasababu yote yanayojitokeza ni mambo ambayo yamejitokeza kwa muda mfupi na yameleta tija kwa watanzania.

“Tunapozungumzia uboreshaji wa sekta ya elimu msingi na sekondari namna ambavyo shule za msingi na sekondari zimeboreka.

Leo tunapozungumza kwenye uboreshaji wa shule za msingi zinazozingatia takwa maalum la Watoto wadogo (kindergarten) kupata eneo la kujifunzia hili nijambo kubwa sana na lenye tija katika nchi yetu.

/ Published posts: 1941

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram