
Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma ametoa wito kwa viongozi na jamii kuunga mkono safari ya mageuzi kwenye kazi za sanaa kwani inaleta matumaini makubwa.
Mwinjuma ameeleza hayo wakati wa Kikao kazi cha 15 cha Maafisa Utamaduni na Maafisa Maendeleo ya Michezo Tanzania, Aprili 22, 2025 jijini Dar es Salaam.
Akiyataja mafanikio ya sekta ya sanaa, ameeleza kuwa uanzishwaji wa Makampuni binafsi yatakayokuwa na jukumu la kukusanya na kugawa Mirabaha kwa pamoja yaani Collective Management organazations (CMOs) Vilevile Mabadiliko Sheria yaliyopelekea Chanzo kingine kipya cha mapato kijulikanacho kama Tozo ya Hakimiliki ambapo zimekusanywa Bilioni 1.47 ikiwa ni jumla ya Mwaka wa fedha 2023/2024 na hadi kufikia Mwezi Machi 2025.
“Tozo ya Hakimiliki inakusanywa kwenye uingizaji wa vifaa vinavyotumika kuzalisha, kubeba na kusambaza kazi za wabunifu. Kupitia chanzo hiki COSOTA kwa mwaka 2023/2024 ilifanikiwa kukusanya jumla ya TSh. 847,985,594.26 na mwaka huu Fedha 2024/2025 hadi kufikia mwezi Machi, 2025 COSOTA imekusanya TShs.628,417,871.69 na hivyo kuwa na jumla TShs, 1,476,403,465.95 ambapo fedha hizo zitagawanywa kwa Mfuko wa Utamaduni na Sanaa 10%, Serikali10%, CMO’s 60% na COSOTA 20%.” Mhe. Mwinjuma