14 views 52 secs 0 comments

WAMACHINGA,BODABODA WAPINGA KUJIHUSISHA NA MAANDAMANO YA CHADEMA

In BIASHARA
April 21, 2025

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA

Wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama Wamachinga na waendesha bodaboda na bajaji wametakiwa kuacha kujihusisha na maandamano bali waendelee kudumisha umoja na kutetea amani ya nchi.

Wito huo umetolewa leo Aprili 21,2025 na viongozi wa wafanyabiashara hao wakati wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.



Makamu Mwenyekiti wa Wamachinga wa Kariakoo na Tanzania, Steven Lusinde, amesema Rais Samia Suluhu Hassan ametoa njia ya maridhiano na kushauri kama kuna changamoto zozote za kiuchaguzi ni vema wahusika wakafuata njia ya maridhiano kuliko kupanga mbinu ambazo zinaweza kuleta uvunjifu wa amani. “Walitutaja kwamba tuwe sehemu ya maandamano tarehe 24, tunajitokeza hadharani kukataa maandamano hayo na tunatoa rai kwa wafanyabiashara tukiamka siku hiyo tukatafute riziki kuhakikisha tunatoka hapa tulipo tunamuunga mkono mheshimiwa rais kwa kuwa walipakodi wa baadaye.



“Watafute maeneo ya wazi wakafanye mikutano yao lakini si kuja kwenye sehemu zetu za biashara, nchi yetu ni ya amani tuendelee kufanya shughuli zetu kila siku na nchi yetu iendelee kuwa na amani,”amesema Lusinde.



Naye Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Bodaboda na Bajaji Mkoa wa Dar es Salaam na Taifa, Said Kagomba, amesema wanatambua athari za maandamano ambayo hayana amani na kuwasihi wafanyabiashara wenzake wasiandamane. “Maisha ya Machinga na Bodaboda na Bajaji ni ya barabarani ndiko tunakopatia riziki, kwahiyo hatuko tayari kuandamana tusimame katika mustakabali wa umoja wetu na kutetea amani na tunu yetu,” amesema Kagomba.

/ Published posts: 1936

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram