15 views 3 mins 0 comments

MBIO ZA RUN FOR BINTI KUREJEA TENA MEI 24 MWAKA HUU

In MICHEZO
April 17, 2025
Mkurugenzi Mtendaji wa Smile For Community Flora Njelekela Akiongea na waandishi wa habari wakati akitoa maelekezo Kuhusu mbio hizo za run for binti

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA

LSF kwa kushirikiana na Shirika lisilo la kiserikali la Smile for Community (S4C) leo limetangaza rasmi msimu wa nne wa mbio za Run for Binti zinazotarajiwa kufanyika tarehe 24 Mei 2025 katika viwanja vya Farasi, Oysterbay jijini Dar es Salaam.



Mbio hizi hufanyika kila mwaka kwa lengo la kuweka nguvu na rasilimali za pamoja katika kuwawezesha watoto wa kike kupata haki ya elimu na afya ya uzazi, Elimu ya Ukatili wa Kijinsia na mbinu za kushughulikia matukio hayo, Elimu ya fedha, na Uhamasishaji wa matumizi ya Nishati safi ili kutengeneza mazingira bora ya kusoma na kupata hedhi salama.

Ameyasema hayo Leo 16 April 2025 Mkurugenzi Mtendaji wa LSF Bi. Lulu Ngโ€™wanakilala Amesema kuwa Katika utekelezaji wa mradi wetu wa Sauti ya Mwanamke, tumeona jinsi wasichana wanavyokutana na changamoto nyingi katika kupata elimu na huduma za afya.



Ushirikiano wetu na Smile for Community pamoja na wadau wetu unalenga kupunguza vikwazo hivi na kuweka njia mpya kwa watoto wa kike.

โ€œKatika utekelezaji wa mradi wetu wa Sauti ya Mwanamke nchini, tumeona dhahiri kwamba wasichana na mabinti wanakumbana na vizuizi vinavyozuilika na visivyoweza kuzuilika katika kupata elimu, huduma za afya, na haki zao za msingi”. Amesema Ng’wanakilala



Aidha Nae Bi. Flora Njelekela ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Smile For Community ameeleza kuwa, Smile for Community kwa furaha kubwa tunatangaza kuwa mbio za msimu huu wa nne zitafanyika tarehe 24 Mei 2025.

“Lengo letu ni kuwafikia watoto wa kike zaidi 2,000 kutoka shule tatu za Mkoa wa Geita na Dar es Salaam kuwawezesha kwa kupitia elimu ya afya ya uzazi, usambazaji wa taulo za kike na ujenzi wa vyoo bora.” Amesema Njelekela



Wadhamini wakuu wa mbio hizo @stanbicbanktz kupitia kwa Mkuu wa Kitengo cha Sekta ya Umma Bi. Doreen Dominic akitoa neno lake mbele ya vyombo vya habari alisema kuwa, “Katika jitihada za Benki ya Stanbic Tanzania tuna hakikisha tunarudisha kwa jamii, tunajivunia kuwa sehemu ya ushirikiano huu. Tunasisitiza kuwa msaada wetu ni endelevu, na tunatumai mbio hizi zitaongeza ufahamu na kuchochea mabadiliko kwa watoto wa kike.”



Wakati huohuo wadhamini wengine wa mbio hizo ambao ni @chatsokotz na @gobaroadsrunners walisema kuwa kupitia mbio za Run for Binti, wanajivunia kuwa sehemu ya tukio hilo linalowawezesha watoto wa kike, ambapo wameeleza kuwa wamejipanga vizuri kuanzia kwenye usajili hadi siku ya tukio lenyewe, ili kuhakikisha washiriki wote wanajivunia kuwa sehemu ya mbio hizo.

/ Published posts: 1928

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram