
Na Mwandishi Wetu
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe Judith Kapinga amesema Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) mwezi Februari, 2022 liliingia makubaliano ya ushirikiano na Shirika la Maendeleo ya Petroli Zanzibar (ZPDC) ambapo kupitia ushirikiano huo masuala mbalimbali yamekuwa yakifanyika kuiendeleza Sektaย ikiwemo kubadilishana ujuzi na utaalam.
Mhe. Kapinga ameyasema hayo leo Aprili 14, 2025 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la la Mbunge wa Kwahani, Mhe. Khamis Yussuf Mussa Mkenge aliyeuliza ni lini Serikaliย itainufaisha Zanzibar katika matumizi ya Nishati ya Gesi ili iweze kutumika katika magari.
“Mheshimiwa Spika katika ushirikiano huu suala la kupeleka gesi Zanzibar ni mojawapo ya agenda kuu. Pande zote mbili bado zinaangalia namna bora ya kufikisha gesi asilia Zanzibar ili iweze kupatikana kwa bei nafuu kwa watumiaji.”. Amesema Mhe. Kapinga