31 views 3 mins 0 comments

NIDA KUSITISHA MATUMIZI YA NAMBA MEI 1 KWA WASIOCHUKUA VITAMBULISHO

In KITAIFA
April 14, 2025
Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya vitambulisho vya TAIFA NIDA James Kaji akizungumza na waandishi wa habari Katika ofisi zao

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA Imesema kuanzia Tarehe 1 Mei 2025 inawafungia matumizi ya Namba Kwa wale ambao hawajajitokeza kuchukua vitambulisho vyao Angali wametumiwa meseji Katika simu zao.

Ameyasema hayo Leo 14 April 2025 Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA James Wilbert Kaji Amesema dhamira yetu na serikali Kwa ujumla ni kuona kila kitambulisho kilichotengenezwa kinachukuliwa na muhusika na hasa ikizingatia vimegharimu serikali pesa nyingi kuvitengeneza

Amesema Tunalazimika kuchukua hatua hiyo baada ya kujiridhisha kwamba wametumia njia mbalimbali kuwafahamisha na kuwahamasisha.wananchi kuchukua vitambulisho vyao tangu tulipovipeleka Katika ofisi za Kata,Vijiji,Mitaa,Vitongoji na shehia.

“Kwa mtu yeyote yule ambaye matumizi ya Namba yake ya utambulisho wa Taifa yatafungwa,hataweza kuitumia namba hiyo Kwa ajili ya huduma yeyote,Ataweza kuitumia tena baada ya kwenda kuchukua kitambulisho chake”Amesema Kaji

Aidha Kaji ametoa Rai kuwa wananchi waliosajiliwa miaka mingi iliyopita na Wana namba tu lakini Bado hawajapata vitambulisho na hawajapokea sms za kuwataka wafike Katika ofisi za Wilaya kuchukua vitambulisho vyao,waende kwenye ofisi za NIDA za Wilaya walikosajiliwa kuuliza kama vitambulisho vyao vimekwisha chapishwa

Kaji Amefafanua kuwa zoezi la kukusanya.vitambulisho na kutuma sms mwezi January 2025 mpaka kufikia Machi 23,2025 jumla ya wananchi 1,880,608 sawa na asilimia 157 ya watu wote waliokuwa hawajachukua vitambulisho vyao,wametumiwa na kupokea ujumbe mfupi wa sms

Pia Amesema wakati vinakusanywa vitambulisho hivyo kutoka ofisi za Kata,vijiji na Mitaa Tulikuwa na vitambulisho 1,200,000 vilivyokuwa havijachukuliwa na wahusika takribani ambao hawajachukua na wametumiwa sms ni 680,608 sms zilizotumwa ni 1,880,608 zimetumwa Kwa waombaji wapya na ambao vitambulisho vyao vimechapishwa tayari.

Kuelekea maagizo ya Mhe Rais, NIDA imeandaa mpango wa usajili na utambuzi wa watu wote wenye umri chini ya miaka 18 kuwezesha upatikanaji wa JAMII NAMBA na Kwa wageni wote wanaoingia nchini na kukaa chini ya miezi Sita,wageni wanaosajiliwa kutambuliwa na kupewa JAMII NAMBA Kwa wanaokaa ndani ya miezi Sita na wenye kibali Cha makazi

Mpango wa usajili wa watu wenye umri chini ya miaka 18 utaanza Kwa majaribio Katika Wilaya tatu ambazo ni Wilaya ya kusini unguja,Kilolo-Iringa na Rungwe- Mbeya Ambapo wanatarajia kusajili jumla ya watu 235,826 ndani ya miezi miwili.

/ Published posts: 1913

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram