
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib mhe, Idrissa Mustafa Kitwana amempongeza Mkurugenzi wa Taasisi ya Twende na Mama kwa maono ya kuanzisha Mashindano ya Dkt Samia & Dkt Mwinyi Cup katika kusapoti jitihada zinazofanywa na Serikali katika kuimarisha michezo nchini.
Mheshimiwa Kitwana amesema kufanya hivyo ni uzalendo wa hali ya juu na itatoa fursa kwa vijana wengi kukuza vipaji vyao na kuimarisha Mahusiano mazuri kwa jamii.
Jaji wa Mahakama ya Kikatiba wa Mali, Maliki Ibrahim Amefunguka kuwa amefurahi kusafiri kwa boti kutoka Tanzania hadi Zanzibar ikiwa ni mara yake ya kwanza kufanya hivyo.
Mbali na hilo amefurahi kuona michezo ikidumishwa kwani ni muhimu katika kuimarisha uhusiano, Pia amesema anafuraha kukutana na Bondia Karim Mandonga na anatamani siku moja awe kama Bondia Mike Tyson.
“Napenda kueleza umuhimu wa kuimarisha uhusiano kati ya Mali na Tanzania kupitia michezo, kwa kuzingatia ari ya Mababa wa Uhuru, kuwaenzi Marais Modibo Keita na Julius Nyerere, ari inayoendelezwa leo na Jenerali Assimi Goita wa Mali na rais Dk. Samia Suluhu Hassan.”
“Ninampongeza bondia Mandonga mwenye kipawa kikubwa na ninatumai kwamba siku moja atapanda safu ya mabondia wakubwa kama vile Muhammad Ali, Mike Tyson, na wengine wengi. Asante Sana.”







