
Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA
_Awaeleza jinsi Serikali ya Rais Samia inavyoitekeleza kwa vitendo Dhana ya Utawala Bora ili kustawisha Jamii._
Afisa Tarafa (Gavana) wa Tarafa ya Katerero Ndugu Bwanku M Bwanku alikua mmoja wa Watoa mada kwenye Sherehe ya Uzinduzi wa Wiki ya Wazazi kwenye mkoa wa Kagera wakati wa Kongamano kubwa la Maadili lililofanyika kwenye Ukumbi wa Bukoba Resort uliopo Kemondo ndani ya Tarafa ya Katerero.
Gavana Bwanku aliwasilisha Mada kuhusu Utawala Bora mbele ya mamia ya Wajumbe na kueleza kwa kina Dhana nzima ya Utawala Bora na jinsi Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan inavyotekeleza kwa vitendo dhana hii kwa uwajibikaji wa Serikali kwa umma kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kote nchi nchini ili kuleta ustawi wa jamii na maendeleo ya kiuchumi kama lengo kuu la Utawala Bora.
Maadhimisho ya Wiki ya Wazazi yanaendelea maeneo mbalimbali nchini na katika mkoa wa Kagera Uzinduzi wa Wiki ya Wazazi ulifanyika Juzi Jumamosi tarehe 12/04/2025 kwenye Tarafa ya Katerero ukiambatana na matukio mbalimbali yakiwemo kupanda miti 200 Shule ya Msingi Kanazi B, kutembelea kituo Cha Watoto yatima Bethania Children’s home na kutoa zawadi pamoja na kufanya Kongamamo la Maadili likiwa na watoa mada kutoka taasisi mbalimbali kama Ofisi ya Afisa Tarafa Katerero, Ofisi ya Afisa Elimu wa Mkoa, Ofisi ya RPC (Dawati la jinsia) Mgaga Mkuu wa Mkoa, Udhibiti Ubora Mkoa na Takukuru Mkoa huku mgeni rasmi akiwa Mwenezi wa CCM Mkoa wa Kagera Comrade Hamimu Mahmudu.
Aidha, Gavana Bwanku kwenye sherehe hiyo iliyofanyika ndani ya Tarafa yake, alitoa miti ya matunda na kuigawa kwa Viongozi wa Jumuiya ya Wazazi kutoka kata zote 29 za Bukoba Vijijini ili wakaipande huku akihamasisha kwenda kutunza mazingira kama ilivyo jukumu lake kubwa la Jumuiya hiyo wakati huu Serikali ikihamasisha sana upandaji wa miti kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, ukame, jangwa n.k