28 views 2 mins 0 comments

TAKUKURU PWANI YAWATAKA WANANCHI KUSHIRIKIANA KUPAMBANA NA RUSHWA KATIKA KIPINDI HICHI CHA UCHAGUZI

In KITAIFA
April 03, 2025

Na Madina Mohammed PWANI WAMACHINGA

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Takukuru ya pwani imewataka wananchi kuajibika Katika kupambana na rushwa pia kuisaidia takukuru Katika mapambano hayo ya rushwa katika kipindi hichi Cha uchaguzi mkuu

Ameyasema hayo Leo 03 Machi 2025 Mkuu wa takukuru (M) Pwani Domina Mukama Amesema takukuru imepata nafasi ya kipekee kuwa mkoa wa kwanza kuzindua mbio za mwenge Kwa mwaka 2025, viongozi wengi wamesisitiza kauli mbiu ya mwenge ya mwaka huu WANANCHI WAJITOKEZE KUJIANDIKISHA NA KUPIGA KURA UKIFIKA MWEZI OKTOBA 2025 Na ujumbe wa MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA ujumbe huu umekuwa Kwa kila mwaka wa mwenge wa uhuru lakini lengo kubwa ni kuwahimiza wananchi kushiriki Kwa pamoja na takukuru Katika mapambano dhidi ya rushwa hasa Katika miradi ya maendeleo



Mwenge wa uhuru unazindua miradi mbalimbali ya maendeleo,na miradi hiyo imeekwa na serikali ilikukidhi haya za wananchi wa eneo husika, mwenge unapita kuangalia miradi hii imekidhi matakwa ya serikali wananchi wamepata huduma ilivyokuwa inaitajika na thamani ya mradi halisi, Takukuru Katika ofisi yetu ni kufatilia miradi ya maendeleo Kwa kuzuia vitendo vya rushwa Katika miradi hiyo

Amesema wananchi wanawajibu wa kupambana na rushwa Kwa kuisaidia takukuru Katika mapambano hayo na kutoa elimu ya rushwa wakati wa uchaguzi na wananchi wanaitaji wafahamu rushwa kabla ya uchaguzi wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi



Aidha Mukama amasema takukuru Kwa Sasa wanaelimisha Kwa kutumia QR Code “Kwa mtu yoyote mwenye smart phone akisikani Katika simu yake atapata taarifa mbalimbali zinazohusu takukuru na taarifa zote za mapambano dhidi ya rushwa”Amesema Mukama

“Tunafanya kufatilia miradi ya maendeleo tunatoa taarifa kila robo mwaka Kwa Sasa hivi tunaandaa taarifa ya January, February na Machi tutaelezea mkoa wa pwani tumefanya nini Katika kuzuia Kwa kupambana na vitendo vya rushwa, Katika uelimishaji, Katika uzuiaji na mapambano na kesi mahakamani”Ameongeza Mukama



Mukama ametoa wito Kwa wananchi kuwa washirikiane na takukuru Kwa kutoa taarifa Kwa takukuru tutazichakata na kuzifanyia kazi wanapotoa taarifa wawetayari kwenda mahakamani Kwa kutoa ushahidi mahakamani.

Kauli mbiu ni kuzuia rushwa ni jukumu lako na langu kila mmoja atimize wajibu wake

/ Published posts: 1883

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram