
Jiji la Mwanza limeshuhudia matembezi makubwa na ya kihistoria yaliyoandaliwa na Umoja wa Makundi Mbalimbali chini ya mwavuli wa Generation Samia (GEN-S) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA). Matembezi haya yalifanyika kuelekea Kongamano Kubwa la Wazi la Fursa za Uchumi, likiwa na kaulimbiu “Mgao wa 30% za Samia Kupitia Mfumo wa NeST”.
Zaidi ya washiriki 8,000, wakiwemo vijana, wanawake, na makundi maalum, wamehudhuria matembezi hayo, wakionesha hamasa kubwa katika kujifunza na kunufaika na mgao wa asilimia 30% wa zabuni za serikali kupitia mfumo wa NeST. Kongamano hilo litawapa fursa washiriki kupata elimu na mwongozo wa jinsi ya kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya uchumi wa taifa.
Kongamano hili limeonesha nia ya dhati ya serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kuwawezesha Watanzania kushiriki kikamilifu kwenye uchumi wa nchi kupitia zabuni za serikali.