15 views 6 secs 0 comments

DKT IRENE AWATAKA WATUMISHI KUENDELEZA MAOMBI NA KUTENDA MEMA KUPITIA MFUNGO WA RAMADHAN NA KWARESIMA

In BIASHARA, KITAIFA
March 29, 2025

Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Dkt. Irene Isaka amewataka watumishi kuendeleza maombi na kutenda matendo mema kupitia Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan na Kwaresima ambayo kwa mwaka huu imewaunganisha waumini wa madhehebu ya Kikristu na Waislam.

Amesisitiza hayo jana Jijini Dodoma wakati wa futari iliyoandaliwa na Mfuko na kuhudhuriwa na Watumishi wa Makao Makuu na Mkoa wa Dodoma pamoja na Wadau wa Maendeleo.



“Mfungo wa Mwaka huu umetuunganisha wote Waislam na Wakristu ambapo tunapata mud awa kumuomba Mungu lakini pia kutenda matendo mema, hili litufundishe na tuendelee hivi hata baada ya Mfungo,” alisema Dkt. Isaka.

Akizungumzia huduma na utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote, aliwaomba watumishi kuendelea na jitihada za kuwafikia wananchi na kuwapa elimu ili waweze kujiunga na kuwa na uhakika wa huduma za matibabu wakati wote bila kikwazo cha fedha

/ Published posts: 1877

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram