
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt, Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali ina dhamira ya dhati ya Kuijenga Zanzibar yenye Maendeleo endelevu na huduma bora za jamii ikiwemo Elimu, Afya na Maji Safi na Salama.
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo alipoizindua Sera Mpya ya Maji na Usafi wa Mazingira ya 2025 hafla iliofanyika Hotel ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege , Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe 22 Machi 2025.
Amesema Uzinduzi wa Sera ya Maji ni hatua Muhimu ya kuyafikia Maendeleo yanayotarajiwa na Nchi katika Uimarishaji wa huduma za Upatikanaji wa Maji na nyengine za Kijamii.
Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa Sera Hiyo Mpya ya 2025 itaimarisha Usimamizi wa Rasilimali Maji na itahakikisha huduma za Upatikanaji wa Maji Kwa kila Mwananchi, Kusaidia kupunguza athari Za Tabia Nchi zinazotokana na uchafuzi wa Mazingira.
Rais Dkt.Mwinyi amewahakikishia Wadau na Wananchi kuwa Serikali itaendelea kuweka Miundombinu ili Miji na Vijiji vilivyo mbali na Miji vipate Maji Safi na Salama.
Ameeleza kuwa hatua hiyo itaenda sambamba na kuwashirikisha Wadau na Sekta Binafsi kwa kuifuata Miongozo ya Sera Hiyo Mpya Ili Kuhakikisha Zanzibar inakuwa na Uhakika wa Maji Safi na Salama.
Amesema kuwa uandaaji wa Sera Hiyo ni Utekelezaji wa shughuli zilizoainishwa katika Mpango wa Utekelezaji wa Sekta ya Maji wa 2022 hadi 2027.
Vilevile Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa Sera Hiyo pia itaimarisha Usimamizi wa Rasilimali Maji na kuhakikisha Upatikanaji wa Maji Unguja na Pemba pamoja na Usimamizi wa Maji taka kwa Kuhakikisha Mazingira yanatunzwa Ipasavyo.