
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amejumuika na Wajumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi katika futari aliyoiandaa.
Hafla hiyo ya imefanyika katika Viwanja vya Ikulu Zanzibar, tarehe 22 Machi 2025.
Ameeleza kuridhika kukamilisha Sadaka ya Futari kwa Mikoa yote Mitano ya Zanzibar kwa Mafanikio na kuwashukuru Waumini wa Dini ya Kiislamu na Wananchi kwa kuitikia mialiko yake kwa mahudhurio Makubwa katika Mikoa yote Unguja na Pemba.
Aidha, Dkt.Mwinyi ametumia fursa Hiyo kuwatakia Waumini vwa Dini ya Kiislamu na Wananchi sikukuu Njema ya Idd el fitr.
Rais Dkt. Mwinyi amekuwa na utaratibu wa kufutarisha kila Mwezi wa Ramadhani utaratibu aliouhitimisha leo kwa Viongozi hao wa Chama cha Mapinduzi.