32 views 47 secs 0 comments

WANYAMAPORI WAPAMBA  SIKU YA MISITU DUNIANI

In KITAIFA
March 21, 2025



Na John Mapepele

Kwa mara ya kwanza  katika historia ya maadhimisho ya Siku ya Misitu Duniani ya mwaka huu  hapa nchini yanayofanyika katika viwanja vya Saba Saba Mjini Njombe  Wizara ya Maliasili na Utalii imeandaa maonesho maalum ya mnyororo wa thamani wa sekta ya misitu pamoja na Wanyamapori.

Kwa vipindi tofauti wakikagua maandalizi ya siku ya Misitu Duniani kwenye maonesho Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Pindi chana na Katibu Mkuu Dkt. Hassan Abbasi wamefafanua kuwa Serikali imeamua kuwaleta Wanyamapori katika maonesho hayo ili kutoa hamasa kwa wananchi kupenda utalii wa ndani.

” Tanzania imebarikiwa kuwa na eneo kubwa la misitu takribani asilimia 50 ambalo ni makazi ya Wanyamapori, hivyo tumeamua kuwaleta wanyama  wananchi waweze kupenda kutembelea hivyo kuliingizia taifa letu fedha.” Amepongeza Mhe. waziri

Naye Dkt. Abbasi amewaarika    wananchi  kutembelea maonesho ya Wanyamapori  hao na kwamba  Serikali imetoa fursa ya wanyama hao kuendelea kuwepo katika viwanja hivyo katika siku za mwisho wa juma hata baada ya kilele hapo kesho ili wananchi wengi wapate fursa ya kuwaona.

Mgeni rasmi hapo kesho ni Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kauli mbiu ya kitaifa ya mwaka huu ni ongeza thamani ya mazao ya misitu kwa uendelevu wa raslimali kwa kizazi hiki na kijacho.

/ Published posts: 1883

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram