25 views 12 secs 0 comments

MGOMBEA WA URAIS CHAMA CHA NLD DOYO KUCHUKUA FOMU YA URAIS KESHO

In KITAIFA
March 19, 2025



Mtia nia wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha National League for Democracy (NLD), Mhe. Doyo Hassan Doyo, baada ya kutangaza rasmi nia yake ya kugombea nafasi ya Urais, tarehe 14 Machi 2025, mjini Morogoro, kupitia tiketi ya Chama cha NLD.

Kwa mujibu wa kanuni ya Chama cha NLD, sura ya pili inamtaka mtangaza nia kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo ndani ya Chama siku 14 kabla ya mkutano mkuu ili kutimiza matakwa ya Chama kikanuni.

Hivyo, Mhe. Doyo Hassan Doyo anatarajia kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo ndani ya Chama tarehe 20 Machi 2025 kabla ya mkutano mkuu. Wanachama wa NLD na waandishi wa habari kwa pamoja mnakaribishwa kushiriki katika tukio hili muhimu la kihistoria la uchukuaji fomu, litakalofanyika tarehe 20 Machi 2025, ofisi za Chama cha NLD, Tandika Mtaa wa Lituhi, Jijini Dar es Salaam, mkabala na msikiti wa watoto yatima, kuanzia saa 4:00 asubuhi.

/ Published posts: 1883

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram