7 views 2 mins 0 comments

WATEMBEZI WA MIGUU WATEMBEA KUTOKA KIGOMA MPAKA KIZIMKAZI KUMFATA RAIS SAMIA

In MICHEZO
March 17, 2025

Na Madina Mohammed DAR ES SALAAM WAMACHINGA


Shirika la Kijamii linaloitwa APHI FOUNDATION,  lenye makao makuu Jijini Mwanza linaendelea na matembezi yao ya Hisani waliyoyaratibu na sasa wamevuka Jijini Dar es Salaam na muelekeo ni Visiwani Zanzibar lengo ikiwa nikufika mpaka Kizimkazi alipozaliwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan



Mkurugenzi mtendaji wa Shirika hilo Mwalimu Philip John amesema Msafara wao unaofahamika kwa jina la “URITHI WETU “ni matembezi ya Hisani yaliyotoka mji mkongwe wa Kigoma Ujiji na kuelekea Visiwani Zanzibar yenye lengo la kuhamasisha watu kuhusu utunzaji wa mazingira ikiwemo matumizi ya Nishati Safi na kukumbuka kazi zilizotukuka za Rais Samia

“Matembezi haya tulitembea mikoa 7 mpaka kufika hapa jiji la dar es salaam na Katika msafara Wetu tupo watu 39 wanawake 11 na wanaume 28” Amesema mwalimu John

Amesema matembezi yao yasihusishwe na masuala ya kisiasa hususani kipindi hiki cha uchaguzi mkuu 2025 lengo Lao ni nyakati zote ili kutengeneza na kuhamasisha na kurithisha vizazi vijavyo vya Tanzania urithi huo wa milele




Aidha Mwalimu John Ameelezea kuwa Kwa hisani ya matembezi yao wameweza kupanda miti Kwa kuhifadhi mazingira ya kijani


Msafara huo Jijini Dar es Salaam uliweka kambi katika shule ya Sekondari ya Turiani .

Kwa upande wake Rehema simanguli kutokea Iringa amesema changamoto ni nyingi walizokutana nazo ni kutoka kwa malengelenge kwenye miguu pamoja na kuvimba.

“Lengo letu lilikuwa ni kutembea tuliweza kutembea hivyo mpaka tufika jijini Dar es salaam na hatukutumia usafiri wa aina yoyote” amesema Rehema

Chifu Mtwale isambe kutoka  Himaya ya Buya amAsilia amesema matembezi yalianzia katika eneo lake analofanyia vikao na matembezi hayo yapo kihistoria ya kudumisha mambo mbalimbali ambayo wanadamu alianzia.



Ameongeza kuwa kwenye matembezi hayo kuna vingo wamefanya ikiwemo kupanda miti na kuangali mila za mababu zetu walipopita na vituo ambavyo walipumzika.

Nae Janet Mabusi Mwalimu Mkuu kutoka shule ya sekondari ya Turiani ambapo nipo msafara huo ulipofikia baada ya kutoka kigoma ameishukuru uongozi wa matembezi ya hisani kwa kuweka kambi shuleni hapo kwa wanafunzi watajifunza mengi kutoka kwao hususani kwenye maswala ya mazingira ya upandaji wa miti

/ Published posts: 1826

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram