
Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kupitia Idara ya Habari MAELEZO kwa kushirikiana na Wakala ya Serikali Mtandao (e-GA) inaendelea na kazi ya kukamilisha ujenzi wa mfumo wa Usajili na utoaji wa vitambulisho vya kidigitali kwa Waandishi wa Habari nchi nzima – JOURNALISTS ACCREDITATION & REGISTRATION SYSTEM (JARS).
Hayo yameelezwa na
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa wakati akitoa taarifa kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo miradi iliyotekelezwa na serikali ya awamu ya sita wakati wa mkutano na waandishi wa habari tarehe Machi 16, 2025 katika Bandari Kavu ya Kwala, mkoani Pwani.
Amesema Mfumo huo unalenga kurahisisha, kuongeza uwazi na kuimarisha utendaji kazi wa waandishi wa Habari kwa kuwapatia huduma ya usajili na utoaji wa vitambulisho vya kazi katika maeneo yao bila kulazimika kusafiri kwenda Dodoma au Dar es salaam kupata huduma hiyo.
Amebainisha kuwa Mfumo huo pamoja na mambo mengine utakuwa na uwezo wa kusajili, kuhakiki na kuhifadhi taarifa za waandishi wa habari wote nchini,Mwandishi wa habari atakuwa uwezo wa kujaza taarifa na kuweka mambo muhimu kama vile picha, mahali anapofanya kazi, taarifa za uraia wake n.k.
Pia, Mfumo utakuwa na uwezo kutoa alama za usalama ambazo mtu hawezi kughushi,
Kupitia mfumo huu Mwandishi wa Habari atakua na uwezo wa kuomba na kupata kitambulisho chake physical ID. Mfumo uwe na uwezo wa kuonesha taarifa kwenye ukurasa wa nyuma back-end ambazo zitahakikiwa na kutumiwa na Idara ya Habari kutoa kitambulisho (Press Card) kwa njia ya mtandao.
Mfumo utakuwa na uwezo wa kumpatia mwandishi wa habari taarifa kabla ya muda wa kuisha matumizi ya kitambulisho chake (alert when the ID is about to expire) pia utakua na kumtumia ujumbe mfupi kupitia simu ya mkononi.
Mwandishi anapoomba kitambulisho mfumo utakuwa na uwezo wa kumpatia namba ya malipo โcontrol Numberโ ya kulipia mtandaoni. Pia Mwandishi akishalipia malipo yake yataonekana na kupitishwa na mamlaka husika (approved).
Mfumo utamwezesha Mwandishi wa Habari kupakia nyaraka muhimu kama vile vyeti vya taaluma kwa ajili ya uhakiki (VERIFICATION).
Mfumo uwe na eneo la waombaji wa ndani na nje ya nchi pia uweke vigezo na mambo muhimu ya kupakia (Requirements) kwa waandishi wa nje.
Mfumo utakuwa na mwonekano wa aina mbili (madirisha) kwa ajili ya waandishi wa ndani na wa nje (International)
Mfumo utakuwa na uwezo wa kuhakiki taarifa za waandishi kwa kuunganishwa na mifumo mingine ya serikali kama GePG, NIDA, NECTA, Uhamiaji n.k kwa ajili ya malipo, uhakiki wa vyeti na taarifa (Verification).
Mfumo utakuwa na uwezo wa kuondoa wale wote waliokosa sifa/wasiohuisha taarifa zao pale wanapotakiwa kufanya hivyo.
Mfumo uwezeshe watumiaji kuweka sani mahali panapohusika (Digital signature)
Mfumo uweze kuruhusu taarifa hususani kitaaluma na eneo la kazi kupatikana kwa njia ya msimbo papo (QR CODE).
“Huduma hii ya kupata vitambulisho vya kidigitali itapatikana kwa Waandishi wa habari wote watakaokuwa wamekidhi vigezo vya kitaaluma (Taaluma ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma),”
Na kuongeza kuwa “Mwandishi wa habari atapaswa kujaza taarifa zake na kufuata maelekezo yaliyoko kwenye mfumo ili aweze kujisajili,” ameeleza Msigwa