12 views 3 mins 0 comments

Mbeto :OMO akatae kurithi sera za Savimbi wa Angola

In KITAIFA
March 16, 2025




Na Mwandishi  Wetu , Zanzibar


Kamati Maalum ya Nec Zanzibar, Idara ya Itikaadi, Uenezi na Mafunzo  imemuasa Mwenyekiti  wa ACT  Wazalendo  ,Othman Masoud Othman,  kuepuka fikra zozote za kutamani  kurithi  sera za Kiongozi wa zamani  wa  UNITA, Jonas  Savimbi.

Aidha azma ya kufikia  uamuzi wa kutaka kuweka kando maridhiaono ya kisiasa Zanzibar na kuanzisha mapambano , anaweza kuitia hofu dunia na kuanza kumtazama kwa jicho lenye shaka

Hayo yameelezwa na  Katibu wa Idara  hiyo ya CCM  upande wa Zanzibar, Khamisi Mbeto Khamis,  aliyesema  fikra zozote za kutishia  kuvunja maridhiano ya kisiasa, inakusudia kuchochea fujo na ghasia kuelekea oktoba mwaka huu.

Mbeto  alisema  ni wazi Othman ameshindwa kukiongoza ACT kwa siasa za kisasa, badala yake kauli  zake zinavunja misingi ya demokrasia kwa kutamani urithi wa sera za mapambano.

Alimtaka Mwenyekiti huyo wa ACT kujua  siasa za mapambano zimepoteza maisha  ya watu  wengi huko Angola na Msumbiji wakati wakipigania  uhuru .


“Hadi kiongozi wa kisiasa anapotangaza uamuzi   wa kutamani mapambano  anaelekea kuingia msituni . Kwa  Zanzibar  sijui  atajificha msitu  upi kati ya  Jozani na Ngeezi. Ni wazi ACT  kinazidi kupoteza haiba na amana yake kisiasa kwa   kuiga mrengo hasi na batili “Alisema Mbeto


Alisema kabla ya kuchaguliwa Mwenyekiti wa  ACT , Mbeto  alisema   Othman  hakuwa  Mwanasiasa  bali ni msomi nguli wa sheria  ambaye  sasa inathibitika anapungukiwa na uwezo wa kukiongoza chama chake.

Aidha Mwenezi huyo wa CCM ,alisema katika maisha yake ya siasa Hayati Maalim  Seif  Sharif Haamd ametembea dunia nzima lakini hakukutana na mkasa wa kuzuiwa kwenye uwanja wowote wa Ndege duniani.



“Viongozi wa ACT wanajua amepata  nafasi ya uenyekiti kwa  mizengwe ya Makamo wake Mwenyekiti, Ismail Jussa Ladhu si ridhaa ya wana ACT .OMO anaishi ACT  lakini  wenye  chama hawamkubali”  ” Alieleza.

Mbeto aliongeza kusema hatua yoyote  kwa Mwanasiasa yeyote anayetaka kuiingiza   Tanzania  kwenye machafuko au kurudisha tena matukio ya ulipuaji mabomu , watu kumwagiwa tindikali, viongozi wa dini kuuwawa au kutiwa vilema ,   dola ipo itatimiza wajibu  wake.

“Kiongozi  mwanademokrasia hawezi kutamka anaweka kando siasa za maridhiano  na kujiandaa kwa mapambano . Matamko hayo ni sawa  na kutangaza  janga la  uhalifu.  ‘ Alisisitiza  Mbeto

Hata  hivyo alisema vyama  vyote vya siasa  nchini,  vimesajiliwa kwa mujibu  wa sheria  Namba 5 ya Mwaka 1992,  vitashindanisha sera na kubadilishana madaraka kupitia  demokrasia ya uchaguzi si  kimapambano .

/ Published posts: 1826

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram