UKIMYA WA WATU WEMA

In UCHAMBUZI
March 12, 2025

Na Mwandishi Wetu WAMACHINGA

Aliyekuwa Rais wa Uganda marehemu Idi Amin alitaka kubadilisha jina la Uganda kuwa IDI. Kila mtu katika baraza la mawaziri alikubali. Sababu ni kuwa ‘Walimwogopa’. *Lakini kulikuwa na mtu mmoja, Malyamungu.* Akamwambia Amin “Mhe Rais unaijua nchi inayoitwa Cyprus?” Basi Amin akamuuliza “Hivyo Cyprus ina uhusiano gani na Mabadiliko ya Uganda, Kuwa IDI?” Malyamungu akamjibu “raia wa Cyprus huitwa cypriots, *Ikiwa tutabadilisha jina la Uganda kuwa IDI, hivyo sisi Waganda tutaitwa idiots, na ulimwengu utatuita IDIOTS [ Wapuuzi ], ilhali hatuko hivyo.*

Hivyo Idi Amin alimwangalia na kusema *”Wewe na mimi, ndio wanaume wenye akili zaidi katika baraza zima la mawaziri.* Na jina la nchi litabaki kuwa ni Uganda”. Na kwa hivyo, lilibaki hadi leo!

Kweli ilikuwa ‘Sauti Moja’ ya Malyamungu lakini ilisimamisha mchakato mzima. *Ukimya wa watu wema hufanya uovu kutawala,* nyumba ya jirani ikiwaka moto hakika hauchukui jembe ukalime!

Tutafakari katika maneno haya….

/ Published posts: 1805

Ukurusa rasmi wa gazeti la Wamachinga. #sautiyawanyonge

Twitter
Youtube
Instagram